NAIBU WAZIRI TAMISEMI JOSEPH KAKUNDA AMEWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUWAJIBIKA IPASAVYO
TAREHE 21-02-2018
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mh
Joseph Kakunda amewataka watumishi wa Serikali hasa walimu
kuwajibika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia majukumu yao vizuri
ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Kakunda ametoa kauli hiyo
wakati akipokea nyumba sita za walimu zilizojengwa na shirika la
ECLAT Development pamoja na Upendo association na kuweka jiwe la msingi katika
bweni la wasichana katika shule ya sekondari Emboreti Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara.
Amesema kuwa walimu wanapaswa
kufahamu kuwa kazi ya kufundisha ndio mkataba waliosainiana na Serikali hivyo
Serikali inawataka kutekeleza majukumu hayo kwa ufasaha .
Ameongeza kuwa katika mkoa wa Manyara
waalimu hawafundishi watoto ipasavyo na kuwa wengi wao wanajishughulisha na
shughuli zao binafsi za biashara na kilimo
Mh Kakunda amesema kuwa mpango wa
elimu msingi bila malipo umeamsha ari na moyo wa wazazi na walezi wengi hasa
vijijini kutaka kupeleka watoto wao shule na kusababisha changamoto nyingi
ikiwemo upungufu wa miundombinu,ambapo amewaomba wadau mbalimbali wa
elimu kuungana na Serikali katika kutatua changamoto hizo zinazoikabili sekta
ya elimu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ECLAT
foundation Peter Toima amesema elimu ndiyo ufunguo wa
maisha na ndicho chanzo cha maendeleo hivyo Serikali pekee haiwezi
kufanya kila kitu na ndio maana wao kama ECLAT wameamua kuisaidia .
NAIBU WAZIRI TAMISEMI JOSEPH KAKUNDA AMEWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUWAJIBIKA IPASAVYO
Reviewed by safina radio
on
February 21, 2018
Rating:

No comments