RAIS MSTAAFU WA LIBERIA ELLEN JONSON ASHINDA TUZO YA MWAKA YA IBRAHIM
MONROVIA.
12February, 2018.
![]() |
Rais Mstaafu wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf akishukuru jambo. |
Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.
Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.
Wakati aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia kuiimarisha nchi hiyo.
RAIS MSTAAFU WA LIBERIA ELLEN JONSON ASHINDA TUZO YA MWAKA YA IBRAHIM
Reviewed by safina radio
on
February 12, 2018
Rating:

No comments