CONGO YASEMA KUWA ITAWACHUKULIWA HATUA MAAFISA USALAMA WANAOWAUA WAANDAMANAJI KWA RISASI.



KINSHASA.  
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema kuwa, itaendelea kuwachukulia hatua maafisa wa usalama watakaobainika kuwaua waandamanaji kwa kuwapiga risasi.
Mahakama ya Kijeshi YA Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kauli ho imekuja baada ya Mahakama ya Kijeshi hapo jana kumfunga jela afisa wa Polisi kifungo cha maisha jela kwa kumpiga risasi na kumuua mwandamanaji katika eneo la Mbandaka siku ya Jumapili iliyopita.
Wanaharakati kadhaa wa haki za binadamu huko Mbandaka wamesema wanasikitishwa na namna kesi hiyo ilivyoendeshwa, wakisema kuwa ilikuwa na lengo la kulinda wahalifu halisi wa mauaji hayo.
Hayo yanajiri wakati ambapo polisi mjini Kisangani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema kuwa imewaachilia huru Makasisi watatu wa Kanisa Katoliki waliokamatwa siku ya Jumapili iliyopita, wakiongoza maandamano ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kujiuzulu.
Polisi nchini DRC imekua ikilaumiwa kutumia nguvu za kupita kiasi kwa kutawanya maandamano hayo.

CONGO YASEMA KUWA ITAWACHUKULIWA HATUA MAAFISA USALAMA WANAOWAUA WAANDAMANAJI KWA RISASI. CONGO YASEMA KUWA ITAWACHUKULIWA HATUA MAAFISA USALAMA WANAOWAUA WAANDAMANAJI KWA RISASI. Reviewed by safina radio on February 28, 2018 Rating: 5

No comments