MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA AWATAKA MADIWANI KUTOTUMIA LUGHA ZISIZOFAA
TAREHE 07-02-2018
Mkurugenzi wa
halmashauri ya jiji la Arusha Athuman Kihamia amewataka waheshimiwa madiwani wa
halmashauri hiyo kutotumia lugha zisizofaa wakati wa kushiriki vikao mbalimbali
badala yake washirikiane kwa pamoja katika kutatua matatizo ya wananchi.
Kihamia ameyasema hayo
katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili kwa mwaka 2017/18 ambapo
amesema kuwa kwa bajeti ya halmashauri kwa mwaka ni shilingi bilioni 14.58 huku
mishahara ya tumishi ikiwa ni shilingi bilioni 32.
Naye Kalist Lazaro Meya
wa jiji la Arusha wamewataka madiwani hao kutimiza wajibu wao kama baraza ili
kuweza kuyafikia malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo .
Kwa upande wake diwani
wa Kata ya Ngarenaro Issaya Doita akizungumza katika kikao hicho amesema kuwa
kutokusainiwa kwa baadhi ya mikataba ya vibanda kunasababisha halmashauri hiyo
kukosa mapato ya kutosha .
Awali kabla ya kuanza
kwa baraza hilo madiwani wawili ambao ni
Gaudence Lyimo kutoka Kata ya Kimandolu na Fransis Mbise kutoka Kata ya Muriet
waliapishwa mbele ya Hakimu Krisanta Chitanda kutoka Mahakama ya Hakimu mkazi
Arusha baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwishoni
mwa mwaka jana.
MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA AWATAKA MADIWANI KUTOTUMIA LUGHA ZISIZOFAA
Reviewed by safina radio
on
February 07, 2018
Rating:

No comments