JAJI MKUU PROFESA. IBRAHIM JUMA AWAAGIZA MAHAKIMU WOTE KUTOA NAKALA ZA HUKUMU.


TAREHE 27-02-2018

JAJI MKUU WA TANZANIA PROF. IBRAHIM JUMA

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amewaagiza mahakimu wote nchini kutoa nakala za hukumu bure kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa walengwa.

Prof. Juma ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma ambapo amesema mahakimu hao watakapokutana na kikwazo chochote cha sheria, kanuni au taratibu katika utekelezaji wa agizo hilo wampelekee mapendekezo.

Amesema kuwa kutokana na mradi wa Benki Kuu ya Dunia, unawataka watimize jukumu hilo la kutoa nakala za hukumu bure kwa wananchi kwa kuwa wananchi wengi wanakosa nakala hizo kutokanan na kushindwa kulipia .

Pia, amesema kuwa kwa kuongezeka kwa suala hilo kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuchangia upatikanaji wa haki pamoja na kuwataka mahakimu wote nchini kufanya kazi kwa weledi.



Hata hivyo, amesema kuwa kama kanuni zinatatiza wahakikishe kanuni hizo zinabadilishwa sambamba na kuhakikisha madai yaliyopo wawasililishe kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ili arudishe fedha hizo.

JAJI MKUU PROFESA. IBRAHIM JUMA AWAAGIZA MAHAKIMU WOTE KUTOA NAKALA ZA HUKUMU. JAJI MKUU PROFESA. IBRAHIM JUMA AWAAGIZA MAHAKIMU WOTE KUTOA NAKALA ZA HUKUMU. Reviewed by safina radio on February 27, 2018 Rating: 5

No comments