Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua wazazi watakaobainika kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu badala ya kuwapeleka shuleni kusoma.
MTWARA.
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua wazazi
watakaobainika kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu badala ya kuwapeleka
shuleni kusoma.
![]() |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa |
Hayo yamesemwa na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Kitangari wilayani Newala mkoani Mtwara ambapo amesema kuwa watoto wote
wana haki sawa ya kupata elimu ambapo kwasasa serikali inaandaa mazingira kwa
watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora nchini.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa watoto hao wanapaswa
kusomeshwa kwa kuwa ni viongozi wa baadae katika nyanja mbali mbali za uongozi kama
Mawaziri na Wakuu wa Wilaya ndani serikali ya nchi hii.
Pia, amesema kuwa watoto hao wakisomeshwa watakuwa
wachangiaji wazuri wa maendeleo ya nchi na wala si sehemu ya nchi huku
akiwaagiza watendaji wa vijiji kuwachukulia hatua wazazi wanaowaficha watoto
hao ndani kila mwaka.
Hali Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza kuwa kila mtoto
mlemmavu atolewe na kupelekwa shule kwa sababu serikali inatoa fedha za
kuwahudumia watoto hao wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri za wilaya
wanazotoka.
Hata hivyo, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema
kuwa hakuna sababu ya mtoto mlemavu kuwekwa ndani.
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua wazazi watakaobainika kuwaficha ndani watoto wenye ulemavu badala ya kuwapeleka shuleni kusoma.
Reviewed by safina radio
on
February 28, 2018
Rating:

No comments