Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutumia elimu waliyoipata kukuza uchumi wa Taifa ikiwemo uanzishwaji wa viwanda.
SIMIYU.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan amewataka Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutumia elimu
waliyoipata kukuza uchumi wa Taifa ikiwemo uanzishwaji wa viwanda.
Makamu wa Rais ameyasema hayo katika sherehe za
mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria iliyofanyika katika uwanja wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Aidha, Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa chuo
hicho kwa jitihada zake za kutekeleza maelezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Magufuli hasa katika suala la uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknoloji William Tate Ole Nasha amesema kuwa chuo kikuu huria kimekuwa
muhimili mkuu wa serikali kwa kufuata sera ya elimu ya mwaka 2014.
Katika Mahafali hayo zaidi ya wanafunzi mia tisa
arobaini na moja wamehitimu kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na
nchi za jirani ambapo wanafunzi saba wamehitimu shahada ya uzamivu wa daktari
wa falsafa ya chuo kikuu huria cha Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutumia elimu waliyoipata kukuza uchumi wa Taifa ikiwemo uanzishwaji wa viwanda.
Reviewed by safina radio
on
February 22, 2018
Rating:

No comments