RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA KUTEUA BARAZA LA MAWAZIRI


TAREHE 21-02-2018

Rais mpya wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema sasa umewadia wakati wa kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri huku kukiwa na tetesi kuhusu kuendelea au kutoendelea kubakia Waziri wa Fedha, Malusi Nkanyezi Gigaga.

Akizungumza jana nchini humo Ramaphosa amesema ni wakati wa kutekeleza maneno yake kivitendo na kutafakari kuhusu baraza la mawaziri na masuala mengine.

Ramaphosa aliapishwa kuwa Rais wa Afrika Kusini siku ya Alhamisi iliyopita baada ya chama tawala ANC kumlazimisha Jacob Zuma kujiuzulu kutokana na kashfa kadhaa zilizokuwa zikimuandama katika kipindi cha miaka tisa ya utawala wake.

Wadadisi wa mambo wanasema, Gigaba anapaswa kuchukua maamuzi mazito katika bajeti ili kujaza pengo la upungufu wa pato na pia kukabiliana na nakisi ya bajeti sambamba na kuwasilisha ramani ya kuboresha uchumi uliovurugika wa Afrika Kusini.

RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA KUTEUA BARAZA LA MAWAZIRI RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA KUTEUA  BARAZA LA MAWAZIRI Reviewed by safina radio on February 21, 2018 Rating: 5

No comments