MUIGAI AJIUZULU BAADA YA KUHUDUMU KATIKA SERIKALI YA KENYA KWA MIAKA 6.


NAIROBI.
Taarifa ya Habari ya saa 08:00 usiku, 13 February, 2018.
Profesa Githu Muigai
Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu katika serikali ya nchini huyo.
Akizungumzia uamuzi huo rais wa Kenya Uhuru Kenyata amesema kuwa amepokea kwa majuto uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai,na anamshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu.
Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu profesa Muigai alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi.
Alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha sheria cha Columbia mjini New York na kutoka 1984 alikuwa mwanfunzi katika chuo cha kusomea uanasheria nchini Kenya.
Akiwa mshauri wa serikali katika masuala ya kisheria, Githu Muigai atakumbukwa kwa kuleta sheria za mageuzi katika timu ya uchaguzi nchini Kenya siku chache tu kabla ya uchaguzi kufanyika.
Hata hivyo rais Kenyata amemteua Jaji Paul Kiharara kuwa mwanasheria mkuu mpya wa Kenya.

MUIGAI AJIUZULU BAADA YA KUHUDUMU KATIKA SERIKALI YA KENYA KWA MIAKA 6. MUIGAI AJIUZULU BAADA YA KUHUDUMU KATIKA SERIKALI YA KENYA KWA MIAKA 6. Reviewed by safina radio on February 13, 2018 Rating: 5

No comments