WATU 23 WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIO YA ANGA NCHINI SYRIA

TAREHE 08-02-2018

Mashambulizi ya anga Syria
Image caption
Takriban raia 23 wameuawa hadi sasa katika mashambulio ya anga ya vikosi vya serikali nchini Syria katika eneo la mashariki mwa Ghota karibu na mji wa Damascus,kunakodaiwa kuwa ni ngome ya waasi.
Waangalizi wa haki za binadamu kutoka Uingereza waliopo katika maeneo hayo wameelezea hali hiyo na madhara kwa raia kutokana na mashambulio hayo.
Umoja wa mataifa umetoa wito kusitishwa kwa mapigano hayo mapema iwezekanavyo,ambapo hapo awali majeshi ya Syria yalidai kuwa vikosi vya anga vya Israel vilishambulia ngome za kijeshi zilizopo karibu na mji mkuu Damascus.
Hata hivyo zaidi ya watu 130 hadi sasa wanahofiwa kufa tangu vikosi vya serikali ya Syria vilipoanzisha mashambulizi ya anga siku ya jumatatu wiki hii.

WATU 23 WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIO YA ANGA NCHINI SYRIA WATU  23 WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIO YA ANGA NCHINI  SYRIA Reviewed by safina radio on February 08, 2018 Rating: 5

No comments