Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa Chuo hicho kwa sasa kimejipanga kuanzisha utaratibu wa kozi fupi zitakazo waandaa watumishi wa umma kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.
KAGERA.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Waziri Mkuu
Mstaafu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa Chuo hicho kwa sasa
kimejipanga kuanzisha utaratibu wa kozi fupi zitakazo waandaa watumishi wa umma
kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.
![]() |
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda. |
Mh Pinda ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya
Tawi ya Chuo hicho Mjini Bukoba mkoani Kagera wakati akizungumza na watumishi
pamoja na wanafunzi.
Waziri Pinda amesema kuwa serikali itashughulikia
changamoto zinazokikabili chuo hicho kutokana na uwezo wa kifedha utakaokuwepo
na kuanzisha kozi fupi zitakazo waandaa watumishi wa umma katika ujenzi wa
taifa.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Tawi la Kagera kilianzishwa
mwaka 2000 kikiwa na wanafunzi ishirini na saba ambapo mwaka 2018 kina
wanafunzi mia tano kikiwa kimefanikiwa kuanzisha vituo vya mitihani katika wilayaa za Ngara na Karagwe.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa Chuo hicho kwa sasa kimejipanga kuanzisha utaratibu wa kozi fupi zitakazo waandaa watumishi wa umma kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments