GHANI ALITAKA KUNDI LA TALIBAN KUSHIRIKI KATIKA MAZUNGUMZO YA AMANI.



KABUL.
Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani amelitaka kundi la Taliban kushiriki katika mazungumzo ya amani ili kuiokoa nchi hiyo.
Ashraf GhaniRais wa Afghanistan.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza katika kongamano la pili la mchakato wa amani mjini Kabul linalohudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 20 na mashirika ya kimataifa.
Rais Ghani amesema serikali ya Afghanistan itawalinda wanachama wa Taliban watakaoshiriki katika mchakato wa amani.
Pia ameahidi kuwapatia pasi za kusafiria za Afghanistan, kuwapa ofisi mjini Kabul, kuwaachia wafungwa na kuondoa vikwazo, iwapo watashiriki katika mpango wa kusitisha mapigano.
Wakati huo huo, wanamgambo wa Taliban wamewaua askari polisi watano kwenye shambulizi  lililotokea kwenye eneo la kizuizi kwenye majimbo ya Kandahar na Oruzgan yaliyoko kwenye mpaka wa kusini mwa Afghanistan na Watu 19 wametekwa katika shambulizi hilo.

GHANI ALITAKA KUNDI LA TALIBAN KUSHIRIKI KATIKA MAZUNGUMZO YA AMANI. GHANI ALITAKA KUNDI LA TALIBAN KUSHIRIKI KATIKA MAZUNGUMZO YA AMANI. Reviewed by safina radio on February 28, 2018 Rating: 5

No comments