WANANCHI BURUNDI WALAANI JINSI MCHAKATO WA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI WA KUPIGA KURA YA MAONI YA KATIBA YA BURUNDI.
BUJUMBURA.

Zoezi la kuandikisha wapiga kura
kuelekea kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba nchini Burundi limeripotiwa
kuendeshwa kwa haraka huku raia wakilaani jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa
kimabavu.
Habari zinaeleza kuwa wapiga kura
watakao andikishwa katika zoezi hilo watakuwa na fursa ya kupiga kura katika
kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba inayopangwa kufanyika mnamo mwezi
Mei pamoja na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.
Katika muda usiozidi wiki mbili kutolewa
kwa zoezi hilo kuanzia tarehe 8 hadi 17 Februari,Tume ya uchaguzi imekiri kuridhishwa
na idadi ya watu ambao wamesha jiandikisha.
Tume hiyo imesema hadi Februari 14
asilimia 58 ya wapiga kura waliotarajiwa walikuwa wamesajiliwa lakini upinzani,mashahidi
na vyombo vya habari vya kujitegemea vimeendelea kurusha matangazo yao nchini Burundi
vikishtumu kwamba raia wanalazimishwa kujiandikisha kwa nguvu na tayari
wameanza kufanyiwa vitisho.
Hata baadhi ya raia kutoka mikoani
nchini humo wamebainisha kwamba wanafanyiwa vitisho vya kuuawa na kulazimika
kwenda kujiandikisha kabla ya zoezi hilo kuisha.
WANANCHI BURUNDI WALAANI JINSI MCHAKATO WA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI WA KUPIGA KURA YA MAONI YA KATIBA YA BURUNDI.
Reviewed by safina radio
on
February 16, 2018
Rating:

No comments