AL-SHABAAB YAUWA WALIMU WATATU KWA SHAMBULIZI ENEO LA GARISA, KAUNTI YA WAJIR,KENYA.


NAIROBI.


Washukiwa wa kundi la Al-shabaab wamewauwa walimu watatu siku ya leo katika shambulio lililotekea katika eneo la garisa kaunti ya wajir nchini Kenya.

Kamanda wa jeshi la polisi Stephen Ngetich alfajiri ya leo amethibitisha shambulizi hilo nakusema kuwa licha ya walimu hao watatu kuuawa mwalimu mmoja alijeruhiwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari inashukiwa kuwa wanamgambo wa Al-shabaab wamehama kutoka upande wa mandera na kuweka kambi yao katika eneo la Wajir ambapo wameendelea kufanya mashambulizi mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Februari 12 Polisi waliokota miili mitatu inayosadikiwa kuwa ya wapiganaji wa Al-shabaab waliouawa mapema katika oparesheni ya polisi ya kuzuia shambulizi la magaidi hao katika kambi ya polisi nchini humo.

AL-SHABAAB YAUWA WALIMU WATATU KWA SHAMBULIZI ENEO LA GARISA, KAUNTI YA WAJIR,KENYA. AL-SHABAAB YAUWA WALIMU WATATU KWA SHAMBULIZI ENEO LA GARISA, KAUNTI YA WAJIR,KENYA. Reviewed by safina radio on February 16, 2018 Rating: 5

No comments