Imebainishwa kuwa endapo jamii itamrejea Mungu kwa kufanya maombi ya toba Mungu anapata fursa ya kukaa ndani yao na kuachilia kibali cha kufanya kazi bila kuwepo na kizuizi chochote wala kusumbuliwa na magonjwa.
ARUSHA.
Imebainishwa kuwa endapo jamii itamrejea Mungu kwa
kufanya maombi ya toba Mungu anapata fursa ya kukaa ndani yao na kuachilia kibali
cha kufanya kazi bila kuwepo na kizuizi chochote wala kusumbuliwa na magonjwa.
Huduma ya redio safina kesho kuanzia saa mbili
asubuhi hadi saa sita mchana katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini
Arusha imekuandalia maombi maalumu ya kurejeshwa karibu na Mungu ili uweze kuwatimizia
Baraka zote pamoja na kuwashindia katika maeneo mbalimbali ya maisha.
Aidha kutokana na jamii kuwa mbali na Mungu matatizo
mbalimbali yamekuwa yakijitokeza kama vile kuishi maisha ya kushambuliwa na magonjwa, kufa kwa miradi,biashara,huduma,kutokupata
watoto katika ndoa pamoja na kuishi maisha ya umaskini.
Kwa mujibu wa somo zipo dalili zinazoonesha kuwa mtu
yuko mbali na Mungu kama vile kushuka viwango vya kiroho, kukosa kibali kwa
watu, kufilisika kiuchumi, migogoro kuzidi hadi kwenye nyumba za ibada, kuomba
bila kupokea majibu ya maombi kuanzisha jambo na kukwama njiani, pamoja na kusumbuliwa
na nguvu za giza mara kwa mara.
Hata hivyo kesho maombi rasmi ya urejesho
yatafanyika ikiwa ni sambamba na watu kurudishiwa uzima, nguvu za kiroho, pamoja
na watu wenye mahitaji sugu kuombewa.
Imebainishwa kuwa endapo jamii itamrejea Mungu kwa kufanya maombi ya toba Mungu anapata fursa ya kukaa ndani yao na kuachilia kibali cha kufanya kazi bila kuwepo na kizuizi chochote wala kusumbuliwa na magonjwa.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments