MPANGO ASEMA TANZANIA INA TAKRIBANI WA WAPATAO MILIONI 54.2



DAR-ES-SALAAM.

Waziri wa fedha na mipango Dr Philip Mpango amesema kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 huku asilimia 50 wakiwa na umri chini ya miaka 18.

Dr Philip Mpango Waziri wa fedha na mipango.
Dr Mpango ametoa takwimu hizo leo jijini Dar-es-salaam wakati akizindua ripoti ya makisio ya idadi ya watu Tanzania ambapo amesema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka wa 2021na ifikapo mwaka wa 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.

Amesema kuwa kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani wa watu wapatao milioni 1.6 hapa nchini na kwamba ongezeko hilo linatokana na idadi kubwa ya vizazi vipatavyo  milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani laki nne kwa mwaka.

Waziri Mpango ameongeza kuwa utafiti wa mama na mtoto wa mwaka 2015 /2016 unaonesha kuwa mwanamke wa Kitanzania anazaa watoto watano katika maisha yake yote ya uzazi ambapo matokeo yake idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya sita katika bara la Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya Nigeria,Ethiopia,Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Misri.

MPANGO ASEMA TANZANIA INA TAKRIBANI WA WAPATAO MILIONI 54.2 MPANGO ASEMA TANZANIA INA TAKRIBANI WA WAPATAO MILIONI 54.2 Reviewed by safina radio on February 28, 2018 Rating: 5

No comments