MAMBA APATIKANA KATIKA BWAWA LA KUOGELEA NCHINI MAREKANI

An alligator is dragged from a Florida poolHaki miliki ya pichaOFFICE
Polisi katika jimbo la Florida, Marekani wamesema mamba wa urefu wa futi 11 alipatikana kwenye bwawa la kuogelea la familia moja katika jumba hilo.
Polisi wamepakia picha za mamba huyo mtandaoni.
Wakazi wa Nokomis waliwapigia simu polisi na kuomba usaidizi baada ya kumgundua mnyama huyo.
Afisa wa polisi wa eneo la Sarasota alipakia mtandaoni picha ya afisa wa wanyama aliyeitwa kumnasa akiwa anamburuta mnyama huyo kutoka kwenye maji Jumamosi.
Polisi wanasema mamba huyo alifanikiwa kupita kwenye uzio uliokuwepo na kuingia kwenye bwawa hilo.
MAMBA APATIKANA KATIKA BWAWA LA KUOGELEA NCHINI MAREKANI MAMBA APATIKANA KATIKA BWAWA LA KUOGELEA NCHINI MAREKANI Reviewed by safina radio on April 02, 2018 Rating: 5

No comments