WAZIRI MKUU WA JAPAN SHINZO ABE KUKUTANA NA RAIS TRUMP.
Waziri mkuu wa Japan
Shinzo Abe amesema atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Florida
kati ya tarehe 17 hadi 20 mwezi huu kujadili masuala ya biashara, mpango wa
kinyuklia na makombora wa Korea Kaskazini pamoja na raia wa Japan
wanaoshikiliwa mateka na Korea Kaskazini kwa miongo kadhaa sasa.
WAZIRI MKUU WA JAPAN SHINZO ABE |
Bw Abe anapanga
kukutana na Trump kabla ya kiongozi huyo wa Marekani kufanya mkutano wa
kihistoria na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwishoni mwa mwezi Mei.
Pia amesema kuwa wanahitaji
kuendelea na shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ili ichukue hatua madhubuti
kuachana na mpango wake wa kinyuklia katika rasi ya Korea.
Mwezi uliopita, Trump
aliongeza ushuru dhidi ya bidhaa za bati na chuma zinazoingizwa Marekani kutoka
nje huku Japan ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazoathirika na ongezeko hilo la
ushuru.
WAZIRI MKUU WA JAPAN SHINZO ABE KUKUTANA NA RAIS TRUMP.
Reviewed by safina radio
on
April 02, 2018
Rating:
No comments