BUNGE LA ETHIOPIA LIMEMTEUA ABIYE AHMED KUWA WAZIRI MKUU
Bunge la Ethiopia limemchagua Abiye Ahmed kuwa waziri mkuu wa
taifa hilo la pili barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu kufuatia kuteuliwa
kwake na chama tawala wiki iliyopita.
ABIYE AHMED |
Bw Abiye ameapishwa rasmi leo kuwa Waziri mkuu akimrithi
Hailemariam Desalegn ambaye amejiuzulu wadhifa huo kati kati ya mwezi Februari
baada ya misururu ya maandamano dhidi ya serikali yaliyosababisha vifo vya
mamia ya raia,wengi wao wakiwa ni raia kutoka maeneo ya Oromia na Amhara.
Waziri Abiye mwenye umri wa miaka 42, ndiye mwanasiasa wa
kwanza kutoka jamii ya Oromo kuwa Waziri mkuu huku kukiwa na matumaini kuwa
atatuliza maandamano dhidi ya serikali,yaliyozuka tangu mwaka 2015.
Pia ameahidi kuleta mageuzi, kuanzisha mazungumzo na Eritrea na
kudokeza kuwa utawala wake utavipa vyama vya kisiasa uhuru zaidi na kuwataka
waethiopia walio nje ya nchi kushiriki kikamilifu katika siasa na maendeleo ya
nchi.
Waoromo takriban milioni 100, ambao ndiyo wengi zaidi
Ethiopia wamekuwa wakilalamika kuwa wanatengwa kisiasa na kiuchumi na utawala.
BUNGE LA ETHIOPIA LIMEMTEUA ABIYE AHMED KUWA WAZIRI MKUU
Reviewed by safina radio
on
April 02, 2018
Rating:
No comments