RAIS MAGUFULI AMESEMA KUWA SERIKALI ITAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John
Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme
ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha.
RAIS MAGUFULI |
Mh magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar-es-salaam
wakati akizindua mradi wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi Two wenye thamani
ya shilingi bilioni mia saba na hamsini.
Amesema kuwa uchumi wa viwanda unaotarajiwa na
serikali hauwezi kufanikiwa bila kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha hivyo
jitihada zaidi zinahitajika kufanywa na
serikali ili kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Meg Watts 1400 zinazozalishwa
kwa sasa hadi kufikia Mega Watts 5000 kwa siku za baadaye.
Ameongeza kuwa mradi huo aliouzindua leo unatekelezwa
na serikali ya Japani kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa gharama ya
shilingi bilioni mia saba na hamsini na utapunguza kwa kiasi kikubwa upungufu
wa umeme hapa nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme
hapa nchini Dr Tito Mwinuka amesema kuwa mradi huo utaongeza Mega Watts 240
katika gridi ya Taifa,ambapo pia ameishukuru serikali kwa kutoa fedha na
kufanikisha kukamilika kwa mradi huo.
RAIS MAGUFULI AMESEMA KUWA SERIKALI ITAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME
Reviewed by safina radio
on
April 03, 2018
Rating:
No comments