SARA APEWA SIKU 30 KUHAKIKISHA KUWA MIGOGORO YA ARDHI WILAYANI HANANG' INATATULIWA KWA HARAKA.


MANYARA.

Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara Bi Sarah Msafiri amepewa siku 30 kuhakikisha kuwa anatatua na kuimaliza migogoro yote ya ardhi iliyopo ndani ya Wilaya yake ambayo imekuwa ikikwamisha Shughuli za maendeleo.

Image result for Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Alexander Mnyeti
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Alexander Mnyeti.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Alexander Mnyeti wakati alipokuwa akizungumza na watumishi,na taasisi mbalimbali wilayani Hanang’ ambapo amesema migogogro hiyo baina ya kata na kata ,vijiji na vijiji ndio unaowaathiri wananchi hao kwa kutumia muda wao mwingi katika migogoro badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Bw Mnyeti amesema kuwa kila anayesababisha migogoro ya ardhi anatakiwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi pamoja na muda kutatua migogoro hiyo ambayo whuku wanaosababisha wakiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote kisheria

Awali akisoma risala kwa mkuu wa mkoa  Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa kipindi cha mwaka 2017/18 kulikuwa na jumla ya migogoro  63 ambapo migogoro mingi imetokea baada ya kuanzishwa kwa vijiji vipya mwaka 2014 lakini mpaka sasa tayari migogoro 18 imeshatatuliwa.

Hata hivyo ametaja sababu zingine zinazochangia Migogoro hiyokuwa ni pamoja na Mihtasari iliyounda vijiji hivyo kutofautiana na Government Notice GN, Baadhi ya vijiji kuanzishwa kwa kutumia nyaraka zenye mapungufu ikiwemo mihtasari ya mikutano mikuu, na baadhi ya wawekezaji wa mashamba makubwa kutotumia maeneo yote waliyomilikishwa kisheria.



SARA APEWA SIKU 30 KUHAKIKISHA KUWA MIGOGORO YA ARDHI WILAYANI HANANG' INATATULIWA KWA HARAKA. SARA APEWA SIKU 30 KUHAKIKISHA KUWA MIGOGORO YA ARDHI WILAYANI HANANG' INATATULIWA KWA HARAKA. Reviewed by safina radio on March 14, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.