RAIS MAGUFULI AZINDUA RELI YA KISASA, STANDARD GEORGE IHUMWA DODOMA.
DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amezindua
jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kati ya mwendo kasi ya Standard George
inayotoka Morogoro hadi Dodoma katika eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli. |
Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na
viongozi mbali mbali wa kiseikali wa ndani na nje nchi ambapo amesema kuwa
mradi huo wa awamu ya pili unagharamiwa kwa fedha za watanzania kwa zaidi ya
shilingi trilioni 7.
Aidha, amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuajiri watanzania
zaidi ya elfu thelathini kuwa wafanyakazi wa kudumu na wafanyakazi elfu sita
wasio wa kudumu katika kutekeleza mradi huo.
Pia, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejibu
suala la ajira kwa vitendo ambapo ameeleze miradi mbali mbali mikubwa
iliyoanzishwa na serikali katika kuleta maendeleo ya nchi ikiwemo mradi wa
umeme wa Stilllers George, usambazaji wa umeme vijijini- REA, na ujenzi wa Meli
kubwa katika ziwa Victoria.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuwa wazalendo katika
kulipa kodi ili kuharakisha maendeleo ya nchi huku akiita Mamlaka ya Ukusanyaji
Kodi ya Tanzania-TRA pamoja na kuhakikisha kuwa inatoa elimu kwa wananchi kwa
ajili ya kuondoa tabia ya ukwepaji wa malipo ya kodi.
RAIS MAGUFULI AZINDUA RELI YA KISASA, STANDARD GEORGE IHUMWA DODOMA.
Reviewed by safina radio
on
March 14, 2018
Rating:
No comments