MAHAKAMA NCHINI BRAZIL YAREFUSHA HUKUMU YA RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO LUIZ INACIO LULA DASILVA

TAREHE 25-01-2018


Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeshikilia hukumu ya makosa ya rushwa iliyotolewa dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva, hatua ambayo ni pigo kubwa kwa matumaini yake ya kugombea tena katika uchaguzi wa mwaka huu.

Jopo hilo la majaji watatu limefanya uamuzi wa kauli moja kuwa hukumu yake ya awali ya miaka tisa na nusu jela irefushwe hadi zaidi ya miaka 12.
Lula ambaye ana umri wa miaka 72, ameuambia umati wa karibu watu  elfu kumi kuwa ananuia kugombea uchaguzi wa rais licha ya kikwazo hicho cha mahakama.


Hata hivyo Anatarajiwa kuendelea kupinga hukumu hiyo kupitia mahakama za juu, kwanza katika Mahakama Kuu ya Haki na kisha Mahakama ya Juu kabisa ya Brazil.
MAHAKAMA NCHINI BRAZIL YAREFUSHA HUKUMU YA RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO LUIZ INACIO LULA DASILVA MAHAKAMA NCHINI BRAZIL YAREFUSHA HUKUMU YA RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO LUIZ INACIO LULA DASILVA Reviewed by safina radio on January 25, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.