HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA SIMIYU ZAAGIZWA KUWATUMIA WATAALAM KUPIMA ARDHI.
TAREHE 05-01-2018
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mh Angela Mabula ameziagiza
Halmashauri zote mkoani Simiyu kuwatumia wataalamu wa ardhi kupima maeneo ya
makazi ili wamiliki wa maeneo hayo wapate hati za kudumu.
Mh Mabula ametoa agizo hilo wakati alipotembelea ofisi ya ukaguzi wa ardhi mkoani humo ambayo
itatumika kuhudumia mikoa ya jirani ya Mara
na Shinyanga ili kumaliza migogoro ya ardhi katika mikoa hiyo.
Aidha, Waziri Mabulu amesema kuwa mchakato wa upimaji ardhi mkoani Simiyu haufanyiki
kwa njia inayostahili hali inayosababisha zoezi hilo kuendelea kusuasua hivyo
jitihada za lazima zinatakiwa kufanyika katika zoezi hilo.
Hata hivyo, Bi. Mabula amesema viwanja vya maeneo ya
miji katika mkoa wa Simiyu pia havijapimwa hivyo ameutaka uongozi wa
halmashauri hizo kutoa vipaumbele katika upimaji wa ardhi katika maeneo ya mijini.
HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA SIMIYU ZAAGIZWA KUWATUMIA WATAALAM KUPIMA ARDHI.
Reviewed by safina radio
on
January 05, 2018
Rating:

No comments