WAKAZI WA WILAYA RUANGWA WATAKIWA KUJIUNGA NA ICHF.
TAREHE 02-01-2018
Waaziri Mkuu wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Wilaya ya
Ruangwa kujiuga na Mfuko wa Afya ya Jamii-ICHF ili waweze kumudu gharama za
matibabu bila ya kulazimika kuwa na fedha taslimu.
Waziri Mkuu ametoa wito
huo katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Ruangwa na vijiji
vya jirani.
Aidha, Waziri Mkuu
Majaliwa amesema kuwa serikali imepiga hatua ya uhamasishaji wa wananchi
kutumia mfumo wa Bima ya Afya kwa watu wote ili kila mwananchi aweze kupata
huduma ya afya hata asipokuwa na fedha taslimu.
Hali kadhalika, Mh.
Majaliwa ameongeza kuwa Mfuko wa Bima ya Afya-ICHF ni Mfuko wa watu wote na
huchangiwa mara moja kwa mwaka ambapo mnufaika hupata matibabu bure katika
kipindi chote cha mwaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Andrea Chizue, amesema mpango wa kutoa kadi
za bima ya afya kwa wazee utawasaidia kupata matibabu bure.
WAKAZI WA WILAYA RUANGWA WATAKIWA KUJIUNGA NA ICHF.
Reviewed by safina radio
on
January 02, 2018
Rating:

No comments