WAAMUZI NANE WA TANZANIA WAMETEULIWA KUCHEZESHA MECHI ZA KLABU AFRICA


TAREHE 25-01-2018
Waamuzi tisa kusimamia mchezo wa shirikisho
Image caption
Waamuzi nane kutoka Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mechi za ligi ya Mabingwa Africa na Kombe la Shirikisho.
Waamuzi wanne wameteuliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.
Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank John Komba wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa Soud Idd Lila na mwamuzi wa akiba Israel Omusingi Njunwa Mujuni huku kamishna wa mechi hiyo akitokea nchini Zimbabwe Gladmore Muzambi.
  • Mchezo huo utachezwa kati ya Februari 20 na 21, 2018 nchini Burundi.
Waamuzi wengine wanne wa Tanzania watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Masters Security Services FC ya Malawi dhidi ya Atletico Petroleos de Luanda ya Angola nutakaochezwa kati ya Febriari 20 na 21,2018 nchini Malawi
WAAMUZI NANE WA TANZANIA WAMETEULIWA KUCHEZESHA MECHI ZA KLABU AFRICA WAAMUZI NANE WA TANZANIA WAMETEULIWA KUCHEZESHA MECHI ZA KLABU AFRICA Reviewed by safina radio on January 24, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.