VIONGOZI WA VYAMA VYA CDU NA SPD WANAENDELEA NA MAZUNGUMZO NCHINI UJERUMANI


TAREHE 12-01-2018



Viongozi wa vyama ndugu vya CDU/CSU na chama cha SPD wanaendelea na mkutano wao mjini Berlin kuangalia uwezekano wa kuanzisha mazungumzo juu ya kuunda serikali ya mseto.

Kansela Angela Merkel amesema vyama hivyo bado vinakabiliwa na vizingiti virefu kwenye mazungumzo hayo,ambapo baada ya mazungumzo ya zaidi ya saa 18 makubaliano bado hayajafikiwa baina ya pande hizo.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mazungumzo hayo huenda yakaendelea hadi hii leo Ijumaa tofauti na ilivyopangwa.

 Kansela Merkel anafanya juhudi za kuunda serikali mpya ili kuunusuru mustakabali wake wa kisiasa,ambapo  alionya hapo awali kwamba mazungumzo yatakuwa magumu.

Hata hivyo  kiongozi wa chama SPD Martin Schulz pia amezungumzia juu ya kuwepo vizingiti vikubwa kwenye mazungumzo hayo.



VIONGOZI WA VYAMA VYA CDU NA SPD WANAENDELEA NA MAZUNGUMZO NCHINI UJERUMANI VIONGOZI WA VYAMA VYA CDU NA SPD WANAENDELEA NA MAZUNGUMZO NCHINI UJERUMANI Reviewed by safina radio on January 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.