RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA AMESEMA UCHAGUZI MKUU NCHINI HUMO UTAFANYIKA NDANI YA MIEZI MITANO IJAYO
TAREHE 19-01-2018
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika
katika kipindi cha miezi minne au mitano ijayo.
Mnangagwa ambaye alishika wadhifa wa urais wa Zimbabwe mwezi
uliopita baada ya jeshi na chama tawala Zanu-pf kumshinikiza Robert Mugabe
aliyekuweko madarakani kwa muda kwa miaka 37 ajiuzulu amenukuliwa na
vyombo vya habari akitangaza kwamba, nchi hiyo itaitisha uchaguzi mkuu
miezi minne hadi mitano ijayo.
Rais Mnangagwa amesema kuwa, uchaguzi ujao wa Rais, Bunge na
serikali za mitaa utafanyika katika mazingira huru na ya haki,ambapo rais huyo
pia mwenye umri wa miaka 75 anatazamiwa
kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama tawala cha ZANU-PF.
Wakati huo huo Bw Roy Bennett, kiongozi wa upinzani aliyekuwa
akiishi uhamishoni amefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea
katika jimbo la New Mexico nchini Marekani.
Ajali hiyo ya kuanguka helikopta imewahusisha pia watu wengine
wanne waliokuwa wamefuatana naye akiwemo mkewe na amefariki akiwa na umri wa
miaka 60.
RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA AMESEMA UCHAGUZI MKUU NCHINI HUMO UTAFANYIKA NDANI YA MIEZI MITANO IJAYO
Reviewed by safina radio
on
January 19, 2018
Rating:

No comments