MAGUFULI AMTUMIA RAIS KENYATA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
02-01-2018
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John
Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta
kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu 36 baada ya gari la
abiria kugongana na lori katika barabara ya Nakuru –Eldoret nchini humo hapo
siku ya jana.
Katika salamu hizo rais Magufuli amesema ajali hiyo
imesababisha majonzi makubwa si tu kwa Wakenya bali kwa wananchi wote wa
jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kwa niaba ya watanzania wote anampa pole rais
Kenyata na wananchi wote wa Kenya.
Rais Magufuli amesema kuwa anaungana nao katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi na amewaombea majeruhi wote wapone haraka.
Hata hivyo ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa
tisa usiku,ambapo kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Rift Valley Bw
Zero Arome alisema kuwa madereva wote wawili ni miongoni mwa waliofariki katika
ajali hiyo.
MAGUFULI AMTUMIA RAIS KENYATA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
Reviewed by safina radio
on
January 02, 2018
Rating:

No comments