RAIS MTEULE WA LIBERIA ATAJA VIPAUMBELE VYAKE
TAREHE 03-01-2018
Weah pia ametoa kipaumbele kwa suala la kukarabati miundo mbinu chakavu ya nchi hiyo akisema kuwa barabara ni suhula muhimu kwa ajili ya mawasiliano huku akiwatolea wito Waliberia wanaoishi nje ya nchi kurejea nyumbani ili kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo.
Rais
mteule wa Liberia ameainisha vipaumbele vyake sita katika muhula wake wa urais
wa miaka sita akitoa wito kwa nchi hiyo kuanza kuuza mazao yake nje ya nchi na
kukarabati miundo mbinu chakavu ya nchi hiyo. George Weah aliyasema hayo jana
katika mahojiano yake ya kwanza kuwahi kufanya tangu kushinda kiti cha urais
wiki iliyopita.
Weah
alipata uungaji mkono mkubwa wa vijana na hivyo kumuwezesha kushinda kiti cha
urais kwa kuibuka na zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa katika duru ya
pili ya uchaguzi wa rais wa Liberia.
Rais Mteule wa Liberia amesema kuwa anataka
kuiona nchi hiyo ikiboresha sekta ya kilimo ili kuwawezesha wananchi kuzalisha
chakula chao wenyewe. Aidha amesema kuwa Liberia ina uwezo wa kuuza mazao
yake nje ya nchi iwapo kilimo kitaboreshwa.
Ametolea
mfano wa Ghana na nchi nyingine jirani zinazouza mazao yao nje ya nchi.
Itakumbukwa
kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Waliberia wanategemea kilimo kwa ajili ya kujikimu
kimaisha huku kampuni kubwa ya Sime Darby yenye makao yake nchini Malaysia
ikiwekeza pakubwa huko Liberia katika ulimaji wa zao la mafuta ya mchikichi.
Weah pia ametoa kipaumbele kwa suala la kukarabati miundo mbinu chakavu ya nchi hiyo akisema kuwa barabara ni suhula muhimu kwa ajili ya mawasiliano huku akiwatolea wito Waliberia wanaoishi nje ya nchi kurejea nyumbani ili kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo.
RAIS MTEULE WA LIBERIA ATAJA VIPAUMBELE VYAKE
Reviewed by safina radio
on
January 03, 2018
Rating:

No comments