WATAKAOBAINIKA KUFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA BONDE LA OEVU MTO KILOMBERO KUSHTAKIWA.
TAREHE 03-01-2018
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dk. Steven Kebwe Steven amesema kuwa watu watakaobainika kufanya shughuli zao
katika bonde oevu la mto Kilombero watashtakiwa chini ya sheria ya kuhujumu
uchumi.
Dk. Kebwe ameyasema
hayo wakati akitoa taarifa ya uharibifu wa bonde hilo kwa Naibu Waziri wa Mali
Asili na Utalii Mh Japhet Hasunga na kusema
kuwa tayari watu 20 wameshakamatwa kwa tuhuma za kuvamia bonde hilo na
wengine kufikishwa mahakamani.
Naye Mratibu wa Bonde
Oevu la mto Kilombero Bw Heledi Fauzeri amesema kuwa waliokamatwa waliokamatwa
wakifanya uharibifu ni pamoja na watu wenye mifugo na wakulima wenye matrekta
ambao walitaka kulima katika bonde hilo.
Hali kadhalika, Bw.
Fauzeri ameongeza kuwa eneo la bonde hilo oevu ni kubwa pamoja na mifugo wanaoingia ukilinganisha na idadi ya askari waliopo
katika ulinzi wa eneo hilo hawalimudu.
Kwa upande wake, Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema ni lazima jitihada zifanyike za
kulilinda bonde hilo huku akiagiza wizara na idara zote kuwa na lugha moja
katika kulinda rasilimali za taifa.
WATAKAOBAINIKA KUFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA BONDE LA OEVU MTO KILOMBERO KUSHTAKIWA.
Reviewed by safina radio
on
January 03, 2018
Rating:

No comments