WAZIRI MKUU WA SOMALIA AWAFUKUZA MAWAZIRI WATATU.

TAREHE 05-01-2017

Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire amewafukuza kazi mawaziri wake watatu huku serikali yake ikiwa inakabiliana na changamoto kutoka upande wa upinzani.

Khaire ametangaza majina ya watu watakaopokea nyadhifa za Waziri wa Mambo ya Nje Yusuf Garaad Omar na balozi wa zamani nchini Marekani Ahmed Isse Awad.

Waziri mkuu huyo pia  amembadilisha waziri wa mambo ya ndani na biashara pamoja na waziri wa viwanda,ambapo Abdi Mohamed Sabriye ameteuliwa kuwa  waziri mpya wa mambo ya ndani na Mohamed Abdi Hayr wizara ya  biashara.

Upinzani katika taifa hilo la Pembe ya Afrika, umekuwa ukiishutumu serikali kuhusu matukio ya usalama ya hivi karibuni ukitaka kumuondoa madarakani waziri mkuu.


Kundi la waasi la al-Shabab linadaiwa kuhusika na shambulizi lililotokea mwezi Oktoba mwaka jana, lililoua watu wapatao 512.
WAZIRI MKUU WA SOMALIA AWAFUKUZA MAWAZIRI WATATU. WAZIRI MKUU WA SOMALIA AWAFUKUZA MAWAZIRI WATATU. Reviewed by safina radio on January 05, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.