WAKULIMA WILAYANI SIMANJIRO WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAM WAO.

TAREHE 17-01-2018




Wakulima wa wilaya ya Simanjiro  mkoani Manyara wametakiwa kushirikiana na watalaamu wao hasa wakati huu wanapoelekea katika msimu wa kilimo ili waweze kulima mazao yatakayowaletea faida kiuchumi.

Hayo yameelezwa na afisa kilimo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Bw Losloky Cloudy wakati akizungumza na Redio Safina jinsi wilaya hiyo ilivyojipanga kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo katika kuboresha sekta hiyo ambayo ndio uti wa mgongo kwa wananchi wengi.

Amesema kuwa katika halmashauri ya wilaya ya Simanjiro wananchi wengi ni wakulima na katika msimu huu wa kilimo wao kama wataalamu wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuandaa mashamba,namna ya kuandaa mbegu bora pamoja na mbolea ya kupandia.

Bw Cloudy ameongeza kuwa,ili mkulima aweze kupata mazao mengi na yanayoweza kumletea faida kiuchumi ni lazima afuate kanuni na taratibu za kilimo zinazotolewa na wataalamu wa sekta hiyo kwani wakulima wengi wamekuwa wakifanya kilimo cha mazoea.


Kwa upande wake mtaalamu wa kilimo katika wilaya hiyo Bi Warid Amani amesema kuwa wao kama wataalamu wamekuwa wakitoa elimu ya kilimo kwa wakulima ili kuhakikisha kuwa wanalima kilimo chenye tija hivyo ni vyema wakulima wakafuata elimu na utaratibu wanaopewa na wataalamu wao.
WAKULIMA WILAYANI SIMANJIRO WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAM WAO. WAKULIMA WILAYANI SIMANJIRO WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAM WAO. Reviewed by safina radio on January 17, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.