RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AAHIDI KUBORESHA SEKTA YA AFYA.

TAREHE 12-01-2018


Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Ally Mohamed Shein amesema kuwa serikali yake itaendelea kuboresha sekta ya afya kwenye upatikanaji wa dawa na vifaa vya matibabu kwa kuongeza bajeti katika wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Dr Shein ameyasema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Zanzibar katika maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi yaliyofanyika katika viwanja vya Aman mjini humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli

Amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018 bajeti ya wizara ya afya itaongezeka na kufikia  shilingi bilioni 12,kutoka shilingi bilioni 7 kwa mwka wa fedha wa 2017/2018 lengo likiwa ni kuboresha huduma bora kwa wananchi wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya afya na hospitali.

Aidha rais Shein ameongeza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya afya ni pamoja na kupungua kwa vifo vya akina mama wanaojifungua, ambapo  vimepungua kutoka vifo mia mbili thelathini na saba kwa mwaka wa 2016 hadi vifo mia moja tisini na tano kwa mwaka wa 2017.

Kwa upande wa watoto wachanga vifo vimepungua kutoka 54 kati ya watoto efu moja  kwa mwaka wa 2010/2011 hadi vifo 43 kwa mwaka wa 2016/2017 kati ya watoto elfu moja.


Hata hivyo sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wastaafu,mawaziri wakuu pamoja na viongozi wengine wa dini na kisiasa.
RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AAHIDI KUBORESHA SEKTA YA AFYA. RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AAHIDI KUBORESHA SEKTA YA AFYA. Reviewed by safina radio on January 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.