JAMII YASHAURIWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA.
TAREHE 03-01-2018.
Jamii nchi imeshauriwa
kuanza mwaka wa 2018 kwa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
magumu kwa kuw ajukumu la kuwalea watoto hao ni la kila mmoja.
Ushauri huo umetolewa na msemaji wa kikundi cha Friends of Batuli
Bi Batuli Isaya wakati akitoa misaada mbali mbali ya chakula ,mavazi
pamoja na msaada wa kuvuta majitaka katika kituo cha kulelea watoto yatima cha
Good Hope Kiwawa Children kilichopo wilayani Arumeru kwa lengo la kuwatia moyo na
kuwatatulia changamoto zinazowakabili kituoni hapo katika mwaka huu mpya wa
2018.
Bi Batuli Amesema kuwa ni vyema jamii ikajiwekea utaratibu wa
kushirikiana na wanaharakati wengine katika kutatua changamoto za watoto yatima
kwa kikundi au kwa mtu mmoja mmoja na kuchangishana kidogo kidogo na hatimae
wakaweza kutatua changamoto zinazowakabili watoto yatima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Ombeni Palangyo amesema
kuwa kituo hicho kimekuwa kikiwalea watoto yatima na kuwapeleka shule lakini
bado kina changamoto zinazokabiliwa nazo ikiwemo vifaa vya shule na hivyo
kuitaka jamii kuungana kwa pamoja kujitolea katika kusaidia watoto hao wenye
uhitaji kama walivyofanya kikundi hicho cha friends of Batuli.
JAMII YASHAURIWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA.
Reviewed by safina radio
on
January 03, 2018
Rating:
No comments