BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAKUSANYA BILIONI 85 .

TAREHE 03-01-2018



Bodi ya mikopo ya elimu ya juu hapa nhcini imesema kuwa imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 85 hadi kufikia Disemba mwaka jana kutoka kwa wanufaika wa mikopo ikiwa ni sawa na asilimia 66 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni mia moja na thelathini kwa mwaka wa fedha wa 2017-2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar-es-salaam mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo Bw Abdurazaki Badru amesema kuwa katika zoezi la kuwasaka wadaiwa wa mikopo wamebainika wanufaika wengine elfu ishirini na sita na kufanya wanufaika wa mikopo hapa nchini kufikia laki moja na elfu ishirini na moja.

Amesema kuwa ili kufikia lengo walilojiwekea kwa mwaka wameweka mikakati mbalimbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 13 kwa mwezi hadi shilingi bilioni 17 kwa mwezi.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema kuwa katika kipindi cha miezi sita wamekamilisha shughuli za utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza  takribani elfu thelathini na tatu mia nne na ishirini na nne yenye thamani ya shilingi bilioni mia moja na kumi.


Hata Bw Badru ameongeza kuwa wanafunzi wanaotakiwa kupatiwa mikopo ni laki moja na ishirini na mbili wa mwaka wa kwanza hadi mwaka wa tatu kwa bajeti ya shilingi biloni mia nne na ishirini na mbili. 
BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAKUSANYA BILIONI 85 . BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAKUSANYA BILIONI 85 . Reviewed by safina radio on January 03, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.