DEMBELE KUREJEA UWANJANI

TAREHE 03-01-2017
Barcelona's Ousmane DembeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na Barcelona Ousmane Dembele huenda akarejea kucheza wiki hii baada ya kukaa nje ya uwanja Kwa karibu miezi minne.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye miaka 20 alijiunga na Barca Agosti kwa £96.8m lakini akaumia akichezea klabu hiyo mechi yake ya tatu - dhidi ya Getafe mnamo 16 Septemba.
Dembele alifanyiwa upasuaji nchini Finland.
Sasa, huenda akarejea kucheza dhidi ya Celta Vigo katika Copa del Rey Alhamisi.
Viongozi wa ligi Barcelona kisha watakutana na Levante katika La Liga Jumapili.
Barca ambao wamo alama tisa mbele kileleni kwenye ligi wamepangiwa kukutana na Chelsea hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Februari na Machi.
DEMBELE KUREJEA UWANJANI DEMBELE  KUREJEA UWANJANI Reviewed by safina radio on January 03, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.