MAREKANI YATISHIA KUKATA MSAADA WA KIFEDHA KWA SERIKALI YA PALESTINA.
TAREHE 03-01-2018
Rais wa Marekani
Donald Trump ametishia kukata msaada wa kifedha kwa serikali ya Palestina, kwa
maelezo kwamba Marekani inawalipa mamia ya mamilioni ya dola za kimarekani kwa
mwaka na hakuna chochote inachoambulia na hakuna heshima kutoka kwa taifa hilo.
Katika utamaduni aliojijengea rais wa
Marekani wa matumizi wa mtandao wa kijamii wa twitter kama sehemu yake ya
kutolea matamko , rais huyo amesema kwamba Wapalestina hawana mpango wowote wa
kuwa na mazungumzo ya maridhiano na amani na Israel na kuhoji uhalali wa
Marekani kuendelea kujitoa kwa kiasi hicho.
Mwezi uliopita rais wa Palestina Mahmoud
Abbas alitoa tamko la taifa lake kutokuwa tayari kupokea mpango wowote wa amani
kutoka Marekani, baada ya mji wa Washington kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu
wa Israeli.
MAREKANI YATISHIA KUKATA MSAADA WA KIFEDHA KWA SERIKALI YA PALESTINA.
Reviewed by safina radio
on
January 03, 2018
Rating:

No comments