WAZIRI NDALICHAKO AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KITENGO CHA UNUNUZI CHUO KIKUU MUHIMBILI.

TAREHE 18-01-2018



Waziri wa elimu sayansi tekinolojia na mafunzo ya ufundi Professa Joyce Ndalichako amemsimamisha kazi mkuu wa kitengo cha ununuzi wa chuo kikuu cha afya na sayansi ya tiba Muhimbili (MUHAS) Bw Nuru Mkali ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za kukiuka utaratibu wa ununuzi.

Professa Ndalichako ametangaza uamuzi huo jijini Dar-es-salaam katika mkutano wake na watendaji wa chuo kikuu cha afya na sayansi ya tiba Muhimbili mara baada ya kutembelea chuo hicho,ambapo pia ameiagiza bodi ya MUHAS kuwa makini na watendaji wasiokuwa waaminifu.

Amesema kuwa hakuna kitu kinaumiza na kuudhi kama mtu anayefanya madudu akidhani kama serikali iko usingizini hivyo ameamua mkuu wa kitengo cha manunuzi kusimamishwa kazi mara moja pamoja na watu wengine wanaohusika kufanya manunuzi bila utaratibu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Bi Mariamu Mwafisi amesema kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika kuhusu sakata hilo watendaji wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.


Hata hivyo mtendaji aliyesimamishwa kazi anatuhumiwa kununua vifaa vya chuo kwa kupitia kampuni tatu ambazo zinamilikiwa na mtu mmoja huku baadhi ya vifaa vikinunuliwa bila kuhitajika.
WAZIRI NDALICHAKO AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KITENGO CHA UNUNUZI CHUO KIKUU MUHIMBILI. WAZIRI NDALICHAKO AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KITENGO CHA UNUNUZI CHUO KIKUU MUHIMBILI. Reviewed by safina radio on January 19, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.