BALOZ SEIF ALLY IDD AMESEMA ZANZIBAR INATAMBUA MCHANGO UNAOTOLEWA NA ASASI ZA KIRAIA

TAREHE 25-01-2018


Makamu wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Idd amesema kuwa Zanzibar inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na asasi za kiraia katika maendeleo ya taifa na ipo tayari kufanya kazi na asasi hizo.

Balozi Seif amesema hayo mjini Zanzibar katika kongamano lililokutanisha asasi mbalimbali za kiraia visiwani humo lengo likiwa ni kujadiliana na kubadilishana uzoefu na kuona namna ya kuziendeleza asasi hizo.

Amesema kuwa ni wazi kwamba pale penye ushirikiano mzuri baina ya serikali na asasi kiraia maendeleo kwa urahisi zaidi na siku zote serikali na asasi hizo zinajenga nyumba moja na mafaniko yao ndio mafanikio ya wananchi.


Kwa upande wake mkurugenzi wa TAMWA kutoka Zanzibar Bi Mzuri Issa amesema kuwa asasi za kiraia ziko tayari kufanya kazi na serikali kinachotakiwa ni ushirikiano na kupitia kongamano hili wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuziendeleza asasi hizo kwa kubadilishana uzoefu.
BALOZ SEIF ALLY IDD AMESEMA ZANZIBAR INATAMBUA MCHANGO UNAOTOLEWA NA ASASI ZA KIRAIA BALOZ SEIF ALLY IDD AMESEMA ZANZIBAR  INATAMBUA MCHANGO UNAOTOLEWA NA ASASI ZA KIRAIA Reviewed by safina radio on January 25, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.