WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MAREKANI YATANGAZA KUZUIA DOLA MILIONI 65 .
TAREHE 17-01-2018
Wizara
ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza kuwa itazuia kiasi cha dola milioni 65
kati ya dola milioni 125 ilizopanga kutoa kama mchango wake kwa ajili ya
ufadhili katika shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada wakati wa
masuala ya dharura.
Wizara
hiyo ya mambo ya nje ya Marekani imesema misaada yoyote itakayotolewa katika
siku zijazo sasa itategemea iwapo shirika hilo litafanya mabadiliko makubwa
katika utendaji wake.
Licha
ya tangazo hilo Marekani bado inatarajia kuidhinisha kiasi cha dola milioni 60
ili kuzuia shirika hilo lisipungukiwe na fedha kabla ya kufikia mwishoni mwa
mwezi huu.
Marekani
imesema bado inasubiri uamuzi kuhusiana na kile ilichoeleza sera zinazoeleweka
kuhusiana na Palestina kabla ya kuidhinisha malipo zaidi.
Marekani
ndio mfadhili mkuu wa shirika hilo ikitoa karibu asilimia 30 ya bajeti ya kila
mwaka ya shirika hilo ambalo pia uhudumia kiasi ya wapalestina milioni 5
waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo wa muda mrefu kati ya
Palestina na Israel.
WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MAREKANI YATANGAZA KUZUIA DOLA MILIONI 65 .
Reviewed by safina radio
on
January 17, 2018
Rating:

No comments