NAIBU WAZIRI WA UJENZI ELIAS KWANDIKWA AMEITAKA TANROADS KUHAKIKISHA WANAWEKA MIZANI YA KUHAMISHIKA KATIKA ENEO LA MAKAMBAKO

TAREHE 19-01-2018


Naibu waziri wa ujenzi Mh Elias Kwandikwa amewaagiza Wakala wa barabara hapa nchini TANRODS kuhakikisha kuwa ndani ya mwezi mmoja wanaweka mizani ya kuhamishika katika eneo la mizani la Makambako ili kutatua changamoto ya msongamano wa magari katika eneo hilo.

Mh Kwandikwa ametoa maagizo hayo  mkoani Njombe mara baada ya kutembelea mizani hiyo na kujionea changamoto ya foleni ya magari katika eneo hilo.

Aidha naibu waziri huyo amewaonya madereva wote wanaotumia kisingizio cha uwepo wa foleni katika mizani hiyo na kufanya mambo yao binafsi.


Hata hivyo Mh Kwandikwa amemaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Lindi,Ruvuma,Mtwara na Njombe ambapo ameweza kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na wizara yake.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI ELIAS KWANDIKWA AMEITAKA TANROADS KUHAKIKISHA WANAWEKA MIZANI YA KUHAMISHIKA KATIKA ENEO LA MAKAMBAKO NAIBU WAZIRI WA UJENZI ELIAS KWANDIKWA AMEITAKA TANROADS KUHAKIKISHA WANAWEKA MIZANI YA KUHAMISHIKA KATIKA ENEO LA MAKAMBAKO Reviewed by safina radio on January 19, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.