BOLASIE AANZA MAZOEZI RASMI

TAREHE 23-11-2017
Mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie amerudi katika mazoezi baada ya miezi 11 akiuguza jeraha.
Image caption
Mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie amerudi katika mazoezi baada ya miezi 11 akiuguza jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata jeraha baya wakati klabu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United mnamo mwezi Disemba 4, 2016 na hadi kufikia sasa amefanyiwa upasuaji mara mbili.
Raia huyo wa DR Congo alifanya mazoezi na timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 wiki iliopita kabla ya kujiunga na kikosi kikuu siku ya Jumatano.
Klabu hiyo imesema kuwa alipokea pongezi kutoka kwa wachezaji wenza baada ya kurudi.
Bolasie ameichezea klabu hiyo mara 15 tangu ahamie kutoka Crystal palace 2016.
BOLASIE AANZA MAZOEZI RASMI BOLASIE AANZA MAZOEZI RASMI Reviewed by safina radio on November 23, 2017 Rating: 5

No comments