WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MH. LUHAGA MPINA AMEWATAKA WANANCHI MKOANI KAGERA KUANZISHA MIRADI YA UFUGAJI SAMAKI.

2-11-2017

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina amewataka wananchi Mkoani Kagera kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo.

Akizungumza mkoani humo alipotembelea kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha VIC Waziri Mpina amesema upatikanaji wa samaki umekuwa mdogo kutokana na wananchi kutotilia manani katika  uzalishaji wa samaki.

Aidha, Waziri Mpina amemuagiza mwekezaji wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja kiwanda chake kiwe kinazalisha tani sitini za uwezo wa uzalishaji wake wa minofu hiyo.

Hata hivyo, amekitaka kiwanda hicho kuongeza uzalishaji kutoka tani kumi na saba za sasa hadi kufikia tani ishirini na tano.
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MH. LUHAGA MPINA AMEWATAKA WANANCHI MKOANI KAGERA KUANZISHA MIRADI YA UFUGAJI SAMAKI. WAZIRI  WA  MIFUGO  NA  UVUVI  MH. LUHAGA  MPINA AMEWATAKA  WANANCHI  MKOANI  KAGERA  KUANZISHA  MIRADI  YA  UFUGAJI  SAMAKI. Reviewed by safina radio on November 02, 2017 Rating: 5

No comments