HALMASHAURI ZOTE HAPA NCHINI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA ELIMU ILI KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA

TAREHE 10-11-2017

Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Joseph Kakunda amezitaka halmashauri zote hapa nchini kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ili kukamilisha ujenzi wa maabara za sekondari zinazotakiwa  katika maeneo yao.

Mh  Kakunda  ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge bungeni waliotaka kujua serikali imefikia wapi katika kutekeleza mpango wake wa ujenzi wa maabara,ambapo amesema kuwa kati ya maabara elfu kumi mia tatu thelathini na saba zinazohitajika hapa nchini tayari maabara elfu sita mia mbili themanini na saba sawa na asilimia 60.7 zimeshakamilika.

Ameongeza kuwa ili maabara hizo zikamilike kwa wakati ni vyema halmshauri zote hapa nchini zikashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kukamilisha ujenzi wa maabara hizo zilizobaki ili kuboresha mazingira bora ya kujisomea kwa wananfunzi.


Aidha katika hatua nyingine waziri huyo amesema kuwa katika siku za mbeleni serikali ina mpango wa kutumia sera mpya ya elimu ya mwaka wa 2014 itakayomlazimisha mtoto mwenye umri wa kwenda shule kusoma chekechea mwaka mmoja,msingi miaka 6 na sekondari miaka 4 ili apate cheti cha kuhitimu cha Leaving Certicate.
HALMASHAURI ZOTE HAPA NCHINI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA ELIMU ILI KUKAMILISHA UJENZI WA MAABARA HALMASHAURI ZOTE  HAPA  NCHINI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA  NA WADAU WA ELIMU ILI KUKAMILISHA UJENZI WA  MAABARA Reviewed by safina radio on November 10, 2017 Rating: 5

No comments