MUGABE AJIUZULU WANANCHI WASHEREKEA
22-11-2017
Barua ya kujiuzulu
kwake iliyosomwa bungeni na Spika Jacob Mudenda, ilisema Mugabe amefanya hivyo
kwa mujibu wa katiba, na kwa kuzingatia maslahi ya nchi na ubadilishanaji
madaraka kwa njia ya amani.
Sherehe hizo zilizoanzia
katika chumba walimokuwa wakikutana wabunge zilienea katika mitaa ya mji mkuu
Harare na nchini kote.
Chama tawala cha ZANU-PF ambacho tayari kilikuwa
kimeanzisha mchakato wa kumtimua Mugabe, kimesema aliyekuwa makamu wa rais
Emmerson Mnangagwa ataapishwa hivi karibuni kuwa rais wa mpito hadi uchaguzi
mkuu utakapofanyika mwakani.
Robert Mugabe
mwenye umri wa miaka 93 ameitawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake miaka 37
iliyopita, lakini azma yake ya kumrithisha madaraka mkewe Grace yamesababisha
uingiliaji wa jeshi, ambao umemshinikiza kujiuzulu.
MUGABE AJIUZULU WANANCHI WASHEREKEA
Reviewed by safina radio
on
November 22, 2017
Rating:

No comments