KANISA LASHAMBULIWA MAREKANI NA WATU 26 KUUAWA

TAREHE 06-11-2017
Maafisa  polisi nchini Marekani wamesema kuwa Watu 26 wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha aliyewafyatulia risasi waumini katika kanisa moja jimbo la Texas wakati wa ibada.
Shambulio hilo limetekelezwa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.
Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano nusu asubuhi.
Gavana  wa Texas Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya Texas.
Mshukiwa  ametajwa kuwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.


Hata hivyo Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist Frank Pomeroy, amesema kwamba binti yake wa miaka 14 kwa jina Annabelle ni miongoni mwa waliouawa, ambapo Maafisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi lakini kufikia sasa lengo la mshambuliaji halijabainika.
KANISA LASHAMBULIWA MAREKANI NA WATU 26 KUUAWA KANISA  LASHAMBULIWA MAREKANI  NA WATU 26 KUUAWA Reviewed by safina radio on November 06, 2017 Rating: 5

No comments