SERIKALI KUPITIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI IMESEMA INASHIRIKIANA NA MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI ILI KUAJIRI WAFANYAKAZI WASIOKUWA NA HISTORIA YA UHALIFU
TAREHE 13-11-2017
Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi
imesema kuwa imekuwa ikishirikiana na makampuni binafsi ya ulinzi ili
kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanaoajiriwa katika makampuni hayo hawana historia
za kiuhalifu.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu
waziri wa ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Mh
Antony Mavunde wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Mh Ruth Mollel
aliyetaka kujua ni kwa jinsi gani serikali inasimamia makampuni binafsi ya
ulinzi ili kuhakikisha kuwa wale wote walioajiriwa katika makampuni hayo hawana
historia za kiuhalifu.
Mh Mavunde amesema kuwa ushirikiano wa serikali
pamoja na makampuni hayo unaazia kwenye usajili baada ya kupitia na kutathimini
maombi ya kuanzishwa kwa kampuni husika ambapo kazi hiyo hufanywa na jeshi la
polisi kwa kushirikiana na wakala wa usajili wa makampuni hapa nchini (BRELA).
Ameongeza kuwa
serikali inafahamu mchango mkubwa unaotolewa na makampuni ya ulinzi hapa
nchini katika kusaidia jeshi la polisi kulinda usalama wa wananchi na mali zao
kwa kuwa polisi walioko hawatoshi kwa polisi mmoja analazimika kuwalinda watu
zaidi ya elfu moja badala ya watu mia nne na hamsini.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi litaenedelea
kutoa mafunzo kwa makampuni binafsi ya ulinzi,kutoa vitambulisho pamoja na
kutoa ushauri ili kuboresha na kuhakikisha huduma ya ulinzi inatolewa katika
viwango vinavyotakiwa.
SERIKALI KUPITIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI IMESEMA INASHIRIKIANA NA MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI ILI KUAJIRI WAFANYAKAZI WASIOKUWA NA HISTORIA YA UHALIFU
Reviewed by safina radio
on
November 13, 2017
Rating:

No comments