RAIS MPYA WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA ATOA MIEZI 3 KWA WALIOPORA MALI ZA UMA
TAREHE 28-11-2017
Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametoa muda wa
miezi mitatu kwa wale wote waliopora fedha za umma na kuzificha nje ya nchi
kuzirejesha.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne, Mnangagwa
amesema muda huo ukimalizika Februari mwakani, serikali itawakamata na
kuwafikisha mahakamani wale wote ambao hawatakuwa wameitii amri hiyo.
Hayo yanajiri wakati ambao aliyekuwa waziri wa fedha
wa Zimbabwe, Ignatius Chombo ambaye alikuwa amekamatwa na jeshi baada ya
kuchukua mamlaka, akifikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita akikabiliwa na tuhuma
za ufisadi.
Kwa mujibu wa wakili wake, waziri huyo wa zamani wa fedha
wa Zimbabwe anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka
wakati alipokuwa waziri wa serikali za mitaa.
Ignatius Chombo ni miongoni mwa maafisa wakuu wa serikali
ya Zimbabwe waliokamatwa baada ya Robert Mugabe kuzuiliwa nyumbani kwake
mnamo tarehe 14 Novemba mwaka huu.
RAIS MPYA WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA ATOA MIEZI 3 KWA WALIOPORA MALI ZA UMA
Reviewed by safina radio
on
November 29, 2017
Rating:

No comments