Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema viwango vya usimamizi wa mechi katika Ligi Kuu England vimeendelea kudorora mwaka baada ya mwaka.
Hii ni baada ya klabu yake kulazwa 3-1 na Manchester City mechi ya Ligi Kuu England Jumapili .
Wenger anaamini mshambuliaji wa City Raheem Sterling alijiangusha na kupewa penalti ambayo iliwasaidia wenyeji kupata bao la pili.
Kadhalika, anaamini bao la tatu halikufaa kukubaliwa kwani lilikuwa la kuotea.
Mambo yakiwa 1-0, refa Michael Oliver aliwazawadi penalti City baada ya Sterling kuanguka alipokabiliwa na Nacho Monreal wa Arsenal, ambapo Sergio Aguero alifunga penalti hiyo.
Baada ya Alexandre Lacazette kukombolea Gunners bao moja, Gabriel Jesus alifungia City bao la tatu lakini David Silva alikuwa amejenga kibanda ardhi ya Arsenal.
Ushindi huo ulikuwa wa tisa mfululizo kwa City, ambayo ni rekodi kwa klabu hiyo msimu mmoja.
Meneja Pep Guardiola alikataa kuzungumzia maamuzi ya refa na kusema kuwa wallishinda kwa njia bora zaidi," Mhispania huyo alisema. "Wakati mwingine mambo kama haya hutokea.
WENGER ALALAMIKIA WAAMUZI WABOVU LIGI KUU YA ENGLAND
Reviewed by safina radio
on
November 06, 2017
Rating: 5
No comments